Makala

IBRAHIM NJOYA

IBRAHIM NJOYA

Imewekwa na - June 7, 2020

MFALME ALIYEKUWA NA WAKE 600 HADI KUWAANDIKIA WATU WAKE KITABU CHA KUFANYA MAPENZI NA WAKE ZAO.

 

Mfalme Ibrahim Njoya amezaliwa mnamo mwaka 1860 eneo la Bamum katika nchi ya Cameroon. Jina lake la asili ni Ibrahim Mbouombuo Njoya. Mama yake alikuwa anaitwa Mjapdunke na Baba yake aliitwa Nsangu Ibrahim. Baba yake Ibrahim, Nsangu – aliuwawa na watu wa Nso wakati wa vita. Baada ya kifo cha Baba yake, Mama yake Ibrahim (Mjapdunke) alishika madaraka mpaka Ibrahim Njoya alipofikia umri wa kuwa mfalme.Njoya akashika madaraka rasmi mwaka 1886. Ibrahim Njoya alikuwa Mfalme wa 17 wa ngome ya Bamum ambayo ilianza tangu karne ya 14.


Mfalme Njoya alikuwa hodari na mahiri sana, aliposhika tu madaraka alijenga mji mkubwa na wakisasa wenye ngome ndani, mji huo uliitwa Fumbam. Mfalme Ibrahim Njoya alikuwa na wake 600. Mfalme Nyoja alipenda sana kutunza mila na desturi za watu wake. Mfalme


Nyoja alipiga hatua zaidi kuanzisha herufi za lugha ya Bamum ambayo ziliitwa Akauku ambapo herufi hizo zilikuwa 73 kwa idadi. Njoya alitengeneza pia Kalenda ya watu wa Bamum, ramani pamoja na kifaa cha kuchapisha nyaraka mbalimbali. Ilifikia hatua Bamum ilikuwa na nyaraka 8000 za taarifa mbalimbali katika masijala yake. Ibrahim pia alijenga mashine kubwa ya kusaga na kukoboa nafaka, alijenga vyuo vikuu na pia alikuwa na Jeshi kubwa na imara.


Ibrahim Njoya aliandika pia kitabu kikubwa cha tiba asilia, pia aliandika kitabu kingine kilichoeleza wanaume jinsi ya kufanya mapenzi na wake zao. Mfalme Njoya aliweza kuendeleza sana ngome yake na pia alitunza sana mila na tamaduni za watu wake. Watabiri wake walitabiri kuwa watu wenye ngozi nyeupe (wazungu) watakuja na watajaribu kutaka kuipora ngome ya Bamum. Walipofika Wajerumani, Njoya aliweza kuzungumza nao na wakafikia makubaliano ya amani.. Ila walipofika wafaransa, walitaka kuichukua ngome ya Bamum iwe chini yao, ila Nyoja alikataa katukatu. Wafaransa wakaanzisha ghasia, waliharibu mali nyingi sana kama mashine zake za kuchapisha na pia maandiko yote ya tiba asilia za watu Bamum na Mfalme Nyoja baada ya ghasia alichukuliwa na kupelekwa Younde, ambapo ndio mji mkuu wa sasa wa Cameroon.


Baada yamuda wafaransa walimtaka Njoya arudi Bamum kuchukua madaraka yake lakini akubali kuwa chini ya wafaransa, ila Njoya aligoma kabisa na akatamka mbele ya nyuso zao kuwa, iko siku atarudi tena Bamum ila kwa mwili wa mfalme mwingine. Njoya akafariki 1933 na kijana wake wa kiume aliyeitwa Seidou Njimoluh Nyoja alirithi kiti cha baba yake. Seidou alirudi Bamum, akajenga shule Bamum kama heshima kwa baba yake, na pia akafufua nyaraka zote zilizoharibiwa na wakoloni wa kifaransa na maandiko yote ya lugha ya Bamum yakaanza kufundishwa shuleni, hadi leo hii inafanyika hivyo. Hadi leo hii, Ibrahim Njoya anasifika sana barani Afrika kwa kugoma kuwasujudia wakoloni.