Makala

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA UVAAJI WA SUTI

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA UVAAJI WA SUTI

Imewekwa na Mr Hadithi - May 8, 2019

 1. ZINGATIA SIZE NA MUONEKANO WA BEGA

Wakati unachagua suti au unapimwa ili ushonewe suti,jambo la kwanza tazama kama bega la suti unayonunua/kupimwa liwe ni size yako.Kwa sisi wabunifu wa mavazi hususani suti (ZA KIKE NA ZA KIUME) bega ndio kipimo cha kwanza kumpima mvaaji na kupitia bega tunaweza pia kutambua kuwa ulinganifu wa vipimo vingine uko sawa au la.Lakini pia BEGA ndio sehemu ambayo ni ngumu  zaidi na inahitajika umakini mkubwa sana katika kubuni nguo na kuishona kwani bega likikosewa basi suti yote haitomfaa mvaaji. Hivyo nawe unaekwenda kununua suti tafadhari anza na bega.

jacket shoulder

 

 2. ZINGATIA KIPIMO/SIZE YA SUTI INAYOKUFIT VIZURI

 

Pamoja na bega kuwa lenye kukutosha lakini pia jitahidi kuzingatia kipimo cha suti nzima kwa ujumla ikutoshe kwa kukufiti vizuri kabisa.Isikupwaye wala kukubana sana.Lakini pia urefu wa koti na mikono pamoja na urefu wa suruali unao endana na wewe.Hali kadhalika kiuno.Kwa  kawaida kanuni ya uvaaji wa suruali  ni kwamba kiunoni suruali inatakiwa kukutosha kabla hata hujavaa mkanda,mkanda ni ziada tu kama visaidizi vingine kama vile saa,blacelets n.k. Lakini sio eti uvae mkanda kwa sababu kiuno cha suruali ya suit sio saizi yako. Hii itasababisha mikunjo na mituno ya hovyo hovyo na kuharibu utamu wa muonekano wa suti yako.

 

 

3. VAA SHATI NZURI YENYE KIWANGO PAMOJA NA MKANDA NA VIATU VIZURI

Watu wengi hapa huwa wanaharibu muonekano wa suti kwa sababu ya ubahili au kutokujali.Ni bora usivae suti kabisa kuliko kuvaa suti na mkanda wenye matundu yaliyotoboka hovyo na mkanda ukiokatikakatika na kubanduka ngozi au rangi yake,Pia epuka kuvaa viatu visivyo na kiwango. 
 

 4. CHAGUA TAI AMBAYO RANGI YAKE IMEKOLEA ZAIDI YA SHATI

Je,huna uhakika ni tai ipi itakupendeza? As a general rule of thumb, your tie should be darker than your shirt to create balance. Hata hivyo, epuka kuchagua tie ambayo ina michoro au maua yanayofanana na shati,maana itamezwa au kuchafua muonekano kati ya tai na shati. Mfano kwa urahisi kama tie ina dots au maua basi wewe chagua shati ambayo ni plain and vice versa.Hata kama zitakuwa shati na tai ni rangi moja itaweza kuonekana na kupendeza endapo zitapangiliwa kama ifuatavyo, Kwa mfano kama shati na tai zote ni rangi nyekundu,nyeupe,bluu au rangi yoyote, basi kimojawapo kiwe kinang'aa zaidi au kiwe na prints

 

 5. TENGENEZA 'DIMPO' YA TIE KWA USAHIHI NA USAWA

 

tie dimple