Makala

USIUMIZE WATU KWA MAKUSUDI!

USIUMIZE WATU KWA MAKUSUDI!

Imewekwa na Hussein Molito - November 20, 2018

Be Helpful not Hurtful
Kuna binti mmoja alikua anasoma chuo kikuu. Alikua na aibu sana. Hakua na muonekano mzuri usoni na mara nyingi alikua anajitenga na kufuata kilichompeleka chuoni. 
Kuna kundi la vijana watukutu chuoni. Mmoja wa vijana hao alimpiga picha msichana huyo na kwenda kuwaonyeshea wenzake.
Wakaandika kwenye picha hiyo. "kama hujawahi kumuona mtu mbaya,basi angalia picha hii."
Waliisambaza picha ya msichana huyo kwenye magroup yote ya chuoni. na bado wakai print na kuibandika kwenye kabati lake.
ilimuuma sana msichana huyo. Akazidi kukosa amani. Kila mtu aliyemuona walionyeshana vidole huku wakimcheka.
Siku iliyofuata ilikua siku ya mitihani. Msichana huyo hakuonekana chuoni. Mmoja wa wasichana waliokua wanasoma nae darasa moja, alimfuata mvulana aliyempiga picha msichana huyo wakati wanajisomea kujiandaa na mtihani na kumuambia Catty hajafika darasani.
Hajasoma, bali toka siku iliyopita alikua analia tu.
wavulana wengine walipuuza na kucheka. 
Lakini mvulana huyo alijiona ana hatia. Alinyanyuka na kukimbia hadi alipo huyo msichana.
Alimuomba msamaha msichana huyo huku akilia na kujutia kwa kitu alichomfanyia.
Akamwambia kama hatomsamehe basi na yeye hatofanya mitihani hiyo ya muhimu kwao.
kwa mara yakwanza alimuona msichana huyo akimfuta machozi kwa mkono wake. na kukiri kua amemamehe. alijifuta machozi na kuachia tabsamu 
Watu waliwapigia makofi baada ya kuwaona wawili hao wakiingia darasani mbio kuwahi mtihani huku nyuso zao zikiwa na furaha.

NB: Tumia muda wawako kuwa mtatuzi wa tatizo na sio chanzo cha tatizo. kuwa Msaada na sio mtu wa kuwavunja watu moyo.
Maneno ya faraja ni tiba. yanaponya na husababisha upendo kati yetu. 
Usipende kuona binaadamu mwenzako anahangaika ili hali unao uwezo wa kumsaidia. 
usimcheke mtu kwa udhaifu alionao. 
usiutangaze udhaifu wa mtu kwa wengine ili wamecheke.
tumia muda wako kuwa furaha ya wenye huzuni. maana nao wanahitaji faraja kama sie..

LOVE EACH OTHER
BE HELPFUL NOT HURTFUL