ASIA DIGITALI

ASIA DIGITALI

Imeandaliwa na:  George Mosenya
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Chombezo
Ukubwa : 131.36 kB

*******UTANGULIZI.***** . . Maisha ni jinsi unavyoyachagua wewe, ukipenda yawe hivi basi yatakuwa ulivyopanga. Ni jitihada za mwanadamu kujichagulia maisha. . . Asia anajikuta katika uchaguzi wa maisha ya sanaa ya maigizo, maisha ambayo alitegemea yatamkomboa yeye na familia yake ya kimasikini. Akiwa jijini Mwanza. . . Tofauti na matarajio, chaguo lake linamfanya atumbukie katika dimbwi la manyanyaso kijinsia. Manyanyaso yanayomfanya Asia afanye chaguo jingine la kimaisha. Chaguo la kipekee ambalo linamfanya abadili mfumo mzima wa maisha yake. Hakika anayapata maisha mazuri lakini katika njia ambazo hazisimliki ni njia zinazoweza kufanywa na wanadamu wachache sana. . . Njia hizi si salama kwa asilimia zote, kila mjanja ana mjanja wake. Asia anapokutana na mjanja wake mambo yanabadilika tena. Hali ya utata inazuka na sintofahamu inatawala. . . Uamuzi mgumu lazima uchukuliwe ili kujitoa katika janga hili. ASIA DIGITALI ni simulizi nyingine ya tofauti kabisa inayozidi kumchambua George Iron Mosenya kama mtunzi wa aina yake…baada ya mateso ya CHOKORAA, chuki katika HATIA, misukosuko katika KIZUIZI, manyanyaso katika ROHO YA MWISHO, taharuki katika JERAHA LA HISIA……..hii ni zawadi nyingine ya aina yake kutoka kwa mtunzi huyu.