
Awali alipokisikia chakula hiki aliapa katakata kuwa hatathubutu kukionja, Anayaishi maneno ya mama yake kwa miaka mingi pasi na kuyakiuka. Hakitaki chakula wala hafanyi jaribio la kukionja..... Umri wa utoto unaondoka anaingia katika utu uzima, anafanaya jaribio la kuonja kile alichokatazwa... mwoja asali, haonji mara moja.. anaonja tena na tena... chakula kinamkinai anaachana nacho. Anajiwekea kiapo kuwa kamwe hatakihitaji tena chakula kile..... Kosa analolifanya ni kusaliti kile kiapo chako yeye mwenyewe...... Tafadhali twende pamoja kuanzia mwanzo hadi tamati