HESABU ZA MOYO

HESABU ZA MOYO

Imeandaliwa na:  Hussein Molito
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Maisha
Ukubwa : 110.74 kB

Dokta Mputa, ni Daktari mwenye taaluma kubwa. Anafanya kazi kwenye kitango cha Mifupa MOI. Anakumbwa na balaa kubwa katika maisha yake. Hali inayomfaya apoteze ufanisi kwenye kazi yake. Anashuka kutoka Daktari tegemewa, hadi kuwa mlevi asiyefaa kwenye jamii. Hussein Bakari, anajitambulisha katika fani ya mziki kama T Control. Yeye na maisha yake ni picha halisi ya maisha magumu na ya kihuni yaliyopo Manzese mtaa wa fisi. Madhila, Shida, Manyanyaso, Ubakaji na uvunjaji sheria. Ni kawaida kwao. Ikapelekea hata askari kupigwa na kuifanya Manzese kuwa uwanja wa vita kati ya serikali na wananchi. Kijana huyo mdogo anaamua kuisimamisha ndoto yake ya kuifanya Manzese kutoka kwenye eneo lisilo salama kwa maisha, hadi kuwa sehemu ya kujivunia. Si rahisi, anakutana na dhoruba nyingi. Ikiwemo kupelekwa jela kwa kesi yao ya utumiaji madawa ya kulevya. Kipaji chake cha kuimba mziki wa Singeri kinakosa thamani, anaamua kuugeukia uandishi wa riwaya. Je atafanikiwa kutimiza ndoto zake? Ni kweli Manzese itakua sehemu ya kujivunia? Wavutaji bangi na waporaji wataacha? Mziki wa Singeri utatoboa kimataifa? Wakati unajiuliza kuhusu maisha ya T Control, usimsahau Daktari Mputa ambaye maisha yake ni Masikitiko makubwa baada ya kuisotea elimu yake kwa muda mrefu. UNGANA NA MIMI KWENYE KISANGA HIKI CHA KUSISIMUA. HESABU ZA MOYO!