NAKUCHUKIA MH. RAIS

NAKUCHUKIA MH. RAIS

Imeandaliwa na:  Hussein Molito
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Maisha
Ukubwa : 107.51 kB

Maumivu makali yatokanayo na uchungu wa ujauzito unaokaribia kuleta kiumbe duniani, ndio uliomfanya binti wa watu mdogo kabisa aliyebeba mimba kwa hila na udanganyifu kutoka kwa mwanaume mwenye nyadhifa kubwa serekalini . Kilio hicho kilichoambatana na kilio cha mtoto wake wa kwanza mwenye umri wa miaka saba, ndivyo vilikua kero kubwa kwa familia iliyoamua kuwatenga kwa kuwapa chumba, jiko na vyoo vilivyokua ndani kwa ndani huku wakiwekewa uzio wa maneno kwa kukataliwa ruhusa ya kutoka nje bila shughuli maalumu. Kwa huruma ya mtoto wa mheshimiwa, anafanikiwa kutoka chumbani kwake na kuita gari ya wagonjwa iliyokuja kuwachukua na kuwahishwa hospitali. Taswira mpya ya msichana huyo mwenye mabaka kila mahali kwenye ngozi yake ingawaje aliikua anaishi katika familia ya waziri huyo mdogo anayependwa sana na wananchi kuliko kiongozi yeyote Yule, inaanza kubadilika baada ya kupungukiwa kwa kiasi kikubwa sana cha damu huku mtoto wake mdogo akiwa ndio ndugu pekee ambaye anaweza kutafuta damu ilipo baada ya kuambiwa kuwa hapo hospitalini hakuna damu iliyobaki kwenye benk ya damu. Anapata machungu baada ya kuona anampa mtoto wake majukumu mazito huku akifahamu fika kua ni ngumu kumpata mtu atakayeweza kumtolea damu akiwa hafahamiani nae. Kwa ujasiri na akili za kuzaliwa alizokua nazo mtoto huyo, analibeba jukumu hilo bila kujali umri wake katika kuhakikisha anamuokoa mama yake na mdogo wake aliyekua tumboni. JE.. ATAFANIKIWA KUPATA DAMU? KWANINI WAMEKOSA MSAADA KATIKA NYUMBA YA MHESHIMIWA ALIYEJAA HURUMA KWA WANANCHI? NINA MUHUSIKA WA HIYO MIMBA? KWANINI ANAMCHUKIA RAIS WA NCHI YAKE? HAYO NA MENGINE MENGI UTAYAPATA KWENYE RIWAYA HII YA KUSISIMUA...