MWANDISHI MATATANI

MWANDISHI MATATANI

Imeandaliwa na:  Hussein Molito
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Maisha
Ukubwa : 240.36 kB

Sura iliyojaa uchovu pamoja na wekundu wa macho kutokana na kuamka asubuhi huku kiwango cha usingizi kikiwa bado kinamuhitaji aendelee kulala, vyote vilimfanya Molito aonekane dhahiri kuwa alichelewa kulala usiku uliopita. Molito mwanangu. Licha ya kuingia chumbani kwako mapema,lakini bado usingizi hujakuisha tu? sauti ya mama yake Molito ilimfanya mtoto huyo atabasamu huku akijiangalia usoni kupitia camera ya simu yake. Kweli aliona kabisa alikua bado anaonyesha dalili za kutoishiwa usingizi licha ya kuoga na kujisafisha kinywa kwa mswaki. Asubuhi hiyo baada ya kupata chai ya pamoja na familia. Alimuaga mama yake na kumuambia kua anatoka na kwenda kwa rafiki yake aitwaye IKRAM. haya mwanangu, usichelewe sana kurudi nyumbani. Maana hizi nyakati zimeshakua za mashaka. Mama aliongea huku akimwangalia mwanaye kwa jicho la huruma ya uchungu wa uzazi. usijali mama, nitahakikisha nalinda usalama wangu vya kutosha. Sihitaji nikutie mashakani wala kukufanya ujawe na huzuni. Kwakua tu, nakupenda sana. Molito aliongea maneno hayo na kuondoka. Alifunga safari kutoka nyumbani kwao akiwa na begi dogo mgongoni lililokua na daftari lake kubwa aliloandika riwaya aliyoachiwa aiendeleze na Ikram, hivyo alienda kituo cha Basi na kusubiri usafiri utakaomfikisha eneo husika. Siku hiyo ilikua ni siku iliyokua na watu wengi saa kwenye kituo hicho cha mabasi. Hata daladala zilizofika kituoni hapo tayari zilikua zimeshajaza. Ilimchukua nusu saa kusubiria usafiri ambao utakua hauna watu wengi ili awezwe kukaa kwenye siti. Lakini haikua hivyo. Kila gari iliyofika hapo ilikua afadhali gari iliopita kwa ujazaji abiria. Molito alichoka kusubiri. Aliuambia moyo wake kua gari yoyote itakayofika hapo wakati wowote kuanzia muda huo ataidandia, haijalishi itakua imejaa kiasi gani. Kitendo cha kusema na moyo wake ni kama vile alijichulia. Zilikatika dakika ishirini nyingine bila gari yoyote iendayo maeneo aliyokusudia kufika. Ndipo kwa mbali aliweza kuiona gari ikija huku ikiwa imeelemea upande moja. Hali iliyomjulisha tayari ilikua imeshajaa. Aliweza kushuhudia macho ya watu wengi wakilitamani gari hilo. Naye akajipa moyo kua kivyovyote vile gari hiyo endapo itasimama basi na eye atakua miongoni mwa watu watakaoipanda. Kweli gari ikafika na watu kadhaa akiwema yeye waliikimbilia gari hiyo iliyokua imejaa mpaka mlangoni na kulazimisha kupanda. Akiwa kwenye harakati za kugobania gari hiyo, ndipo alipohisi uwepesi kwenye mgongo wake gahfla tu. Aligeuka nyuma na kuweza kumuona mtu akikimbia na begi lake. Alishuka haraka na kujaribu kumkimbiza huku akipiga kelele za kuwajulisha watu kua huyo aliyechukua begi lake ni mwizi. Kwakua kila tu alikua anapigania la kwake, hakuna aliye shirikiana naye kumkimbiza mwizi huyo aliyekua anakimbia kwa spidi kubwa zaidi ya kumtazama tu. Kwakua mwizi alikimbilia maeneo ya Bondeni, watu walimshauri Molitoasimfuate mpaka huko, maana anaweza kumsababishia madhara mengine. Kama si kumuibia vilivyobaki, basi kumdhuru kwa silaha za ncha kali wanazotembea nazo. Safari ya Molito ikaanza kuingia mkosi na kufanya anyongee na ile furaha yake yote kuyeyuka kama vile barafu lileyukavyo pindi liwekwapo kwenye eneo lenye joto kali. Alijikutaka akikaa tu pale stendi huku akiwa amepoteza hata uwezo wa kufikiri na kuchukua maamuzi kati ya kurudi nyumbani au aendelee na safari yake. Wakati akiwa amekaa huku mwili wake wote umekufa ganzi kwa kile kitendo kilichotokea, lilifika gari tupu likisanya kuelekea safari yake aliyoipania. Hapo hapo yalikuja maamuzi ya kwenda tu kwa Ikram hata kama lile daftari aliloandika riwaya yake halipo tena. Alipanda kwenye daladala hilo na kukaa siti ya mbele kabisa. Alisalimiana na dereva wake na kusubiri aondoe gari ili aweze kufika nyumbani kwa kina Ikram amuelezee dhamira ya kwenda kwake na yapi yaliyomsibu pindi alipokua njiani. Alifika nyumbani kwa Ikram na kugonga mlango. Baada ya kubisha hodi kwa sekunde kadhaa. Malngo ulifunguliwa na kupokelewa kwa tabasamu pana na mwenyeji wake. Karibu sana Molito. Ikram aliongea maneno hayo huku akiukomea mlango wake baada ya mgeni wake kuingia. nimeshakaribia kaka.... Za toka tulipoachana hapa nyumbani? Molito aliuliza tena. Namshukuru Mungu usalama upo wa kutosha. Sijui wewe na wazazi wako huko utokapo? Ikram aliuliza na kumfanya Molito atoe majibu huku akijilazimisha kuonyesha tabasamu. wote wazima tu... Leta habari mpya Ikram aliongea hayo na kunyanyuka kuliendea jokofu lililokua hapo karibu na kutoa jagi lililojaa juisi ya embe. Alichukua galsi mbili na kurudi tena kwenye kiti. Alimimina juisi hizo ujazo sawa na glasi moja kumsogezea mgeni wake. hakuna mpya. Japo kuna habari mbili kwa wakati mmoja. Mbaya na nzuri. Molito aliongea maneno hayo baada ya kushukuru kwa kinywaji alichopatiwa wakati huo. anza na habari nzuri. Maana ukisema habari mbaya hata furaha ya kile kizuri haitokuja. Ikram aliongea nakumfanya Molito atabasamu. Habari nzurini kwamba ile riwaya ya Hitaji la Malkia nilikamilisha kuiandika kuanzia pale ulipoishia wewekuiandika hadi mwisho kabisa. Ila habari mbaya kuna mwizi ametokea kuiba begi langu lililokua na daftari lililokua nahio Hadithi ndani. Molito aliongea maneno hayo na kumfanya Ikram atabasamu. pole sana. Ila nakuombakuwa na amani ya kutosha kabisa. Maana Begilako kunamtu amelileta hapa muda siomrefu kabla hujawasili. Ikram aliongea kauli zilizomduwaza Molito. Sijaelewa ulivosema kua kuna mtu amelileta hilo begi... Inamana huyo mwizi aliyeniibia Begi langu anaishi humu? Molito aliuliza. wewe uliibiwa kweli na lengo la mwili lilikua kupatakitu chochotekutoka kwenye begi ili maishayae yaendelee. Ila alichokuja kukutana nacho, ilimfanya mpaka atafute hiinyumba na kulirejesha hilo begi. Ikramaliongea na kumfanya Molito amsikilize wa ummakini. kuna nguvu kubwa sanaipo kwenye riwaya yako uliyoiandika. Hivyo kuanzia leo unatakiwa kuamini kua Salkina yupo kwenye ulimwengu huu na ndiye aliyemshurutisha huyo mwizi hadi kulileta hili Begi hapa nyumbani. Ikram aliongea maneno yaliyomfanya Molito abaki ameduwaa. Ilikua mshangao wa kustaajabisha kwa Molito. Maana alijua fika jina la Salkina aliilitumia yeye kwenye riwaya yake. Na Ikram hajawahi kuisoma riwaya hiyo ukilinganisha na muda ambao alikua akiandika visa hivo hakuwahi kumshirikisha. Amelijuaje jina la Msichana niliyemtumia kwenye riwaya yangu? Na amejuaje kua nimempa nafasi kama Malikia mwenyewe kwenye himaya za Eywa? Na vipi kiumbe niliemuandika tu katika maandishi ya kwene daftari tena kwa kutunga tu na si kwamba ni historia ya zamani kuhusiana kuishi kwa mtu huyo na akatokea kuishi kwenye jamii ya kweli? Hayo maswali na mengine Mengi yaliendelea kujirudikwa kichwani mwa Molito.