CHUMA CHA PUA

CHUMA CHA PUA

Imeandaliwa na:  George Mosenya
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Maisha
Ukubwa : 182.17 kB

RIWAYA: CHUMA CHA PUA KIZA kinatanda mkoani Kigoma, wananchi wanaishi kwa mashaka! Mtu ama kundi la watu wasiofahamika linafanya mauaji bila kutoa sababu zozote za msingi. Serikali imetulia tuli bila kusema lolote hadi pale watoto mapacha wa mkuu wa mkoa wanapotoweka katika mazingira tatanishi. Wale waliopoteza wapendwa wao wanabaki midomo wazi baada ya kukamatwa ili wasaidie upelelezi. _______ Huko mkoani Tabora, bila kutarajia mwalimu Mohameddy (Meddy) aliyeukimbia mkoa wa Kigoma na kuhamia Tabora ili kukaa mbali na kumbukumbu za huzuni za kumpoteza mke na mtoto wake katika janga hilo la ajabu, anakamatwa na kutajwa kuwa anamfahamu muhusika wa mauaji na anajua walipo watoto wa mkuu wa mkoa. Mkuu ambaye alijifanya mungu mtu! Mwenyekiti wa mtaa ambao alikuwa anaishi mwalimu Meddy anaguswa na janga lililomkumba Meddy! Anajivika bomu na kuamua kwenda Kigoma kuusaka ukweli. Kwa majina anaitwa GEZA ULOLE! Mkewe anamzuia lakini kwa maozea yake ya kushinda vita kila akiamua kupambana anatambua kuwa hata hii ni vita ni nyepesi. Akauvaa mkenge! Huku anakutana na adui asiyejulikana, anaua wakati usiojulikana na mbaya zaidi hata sababu za kuua kwake hazijulikana. Adui wa sasa alikuwa ni CHUMA CHA PUA. GEZA ULOLE najikuta akipambana kwa kila namna kwa ajili ya uhai wake, amani ya watu wa Kigoma na zaidi kwa ajili ya familia yake. Je? Ni kipi kilijiri na kutamatisha mkasa huu wa mwisho kabisa wa GEZA ULOLE??? Ingia ndani ujisomee kila kitu. JAZA KIBUBU CHAKO SASA ILI UFURAHIA HADITHI APP!