KONSTEBO NGUZU

KONSTEBO NGUZU

Imeandaliwa na:  George Mosenya
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Upelelezi
Ukubwa : 276.66 kB

RIWAYA: KONSTEBO NGUZU (Mzimu wa babu) Muhtasari! Askari mwenye cheo cha chini kabisa. Cheo cha konstebo aitwaye Martin Nguzu anajikuta pasi na kutarajia safari yake ya kuhamishiwa kituo cha kazi kutoka jijini Mwanza kwenda jijini Dar es salaam inakumbwa na dhoruba kali. Anatua jijini kama askari mtiifu anayeheshimu kiapo chake, lakini anapigwa teke na Zubeda, askari mwenzake ambaye zaidi ya kuwa na cheo cha Koplo alikuwa na sifa nyingine. Alikuwa amejaa huba inayoweza kumyumbisha mwanaume. Konstebo Nguzu anayumba!! Bila kujua kuwa anaangukia katika sahani analokula Inspekta mkorofi, inspekta aliyezikwepa risasi nyingi, inspekta mwenye shabaha.. asiyekuwa na masihara. Inspekta asiyeogopa kuua…. Nguzu hakujua kuwa anapojilaza pembeni akiwa anafarijiwa na Zubeda kuna miguu ya Inspekta mle ndani. Kizaazaa kinazuka pale siri inapotoroka na kujileta hadharani…. Konstebo Nguzu anachomewa ndani ya nyumba aliyokuwa anaishi. Kimya kinatanda na amani inajaribu kurejea bila uwepo wa Konstebo Nguzu. Ukimya ule haukudumu sana kabla halijazaliwa balaa la karne! Ilianza kama vita ya mapenzi, inageuka kuwa vita ya kihistoria…. Endelea ndani katika kitabu hiki cha KONSTEBO NGUZU. Ni zaidi ya riwaya