KIZUIZI

KIZUIZI

Imeandaliwa na:  George Mosenya
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Maisha
Ukubwa : 390.02 kB

Kwa mazungumzo ya kawaida, kwa kutumia pesa na vitisho ikibidi. Kijana mtanashati aliyeneemeka kwa fedha na mali nyingi James Syaga alikuwa amehakikisha kuwa hakitatokea kikwazo chochote cha kumzuia asifunge ndoa na mwanadada Emmy John! Likiwa ni tangazo la mwisho kabisa kanisani kabla ndoa ile haijapewa Baraka za kufungwa. Anatokea Jose B wa ukweli. Kijana fukara, asiyekuwa na elimu ya darasni bali ujanja wa mtaani na kujua mengi. Anagundua kitu kilichofanana na udaku dhidi ya James Syaga. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake anaamua kuitumia tetesi ile kujiingizia pesa dhidi ya bwana huyu mwenye matamanio ya kuoa. Hakuufahamu wadhifa wake, hakuwajua watu waliomzunguka... Jose B akaingia kuicheza ngoma asiyoijua! Kile kizuizi alichodhani ni biashara nyepesi kinageuka kuwa mtihani aliotamani nyakati zirejee nyuma asithubutu kuufanya... Lakini tayari maji alishayavulia nguo... IFUATILIE KUANZIA MWANZO HADI MWISHO...