ALICE THE SUPERSTAR

ALICE THE SUPERSTAR

Imeandaliwa na:  Hussein Molito
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Mapenzi
Ukubwa : 150.76 kB

ALICE THE SUPER STAR NA HUSSEIN O. MOLITO 0718 97 56 59 / 0765 68 48 70 INTRODUCTIONS: Sauti ya mwanadada aliyebarikiwa kila aina ya vipaji ambavyo kwa pamoja anavitendea haki vipaji vyake, ndio iliyonifanya mimi nitamani kumsikiliza kila niisikiapo sauti yake. Si mimi tu niliyeiona thamani ya sauti ya mwana dada huyo, ila kila mvulana alisikiapo jina la ALICE, basi moyo wake ulikiri uzuri wa kila kitu alichojaaliwa mrembo huyo. Napenda anavyotangaza, napenda anavyoimba, napenda anavyoigiza pia napenda kumtazama kila nimuonapo kwenye mabango ya matangazo mbali mbali ambayo makampuni mengi yalikua yana mtumia mrembo huyo kwenye kuvutia biashara zao. Ilifikia kipindi mpaka kampuni inayotengeneza sabuni, waliamua kutumia jina lake na picha yake kwenye sabuni hiyo iliyo pewa jina la Alice. Hapo waliweza kunipata kwa kuitumia sabuni hiyo tu, si kwa sababu ni nzuri kuliko sabuni zote, ila Alice alikua ni mzuri kuliko kitu chochote katika mboni za macho yangu. Geto langu limejaa picha zake nilizokata kwenye magazeti mbali mbali, hadi kufikia wakati nilitamani kwenda kwenye tamasha lolote ambalo nitasikia Alice ata perform japokua kipato changu kidogo. Sikuweza kuamini macho yangu siku nilipokutana na Alice macho kwa macho huku tabasamu zito lililojaa bashasha likiwa linanilenga mimi. Niliishiwa nguvu hadi kauli baada ya kuona superstar huyo akiwa mbele yangu na kunitazama kwa macho yake malegevu. Kwa mara ya kwanza nilipata nafasi ya kugusanisha mikono yangu na mikono yake. “nimesikia wewe ni fundi mzuri… nimekutafuta sana LARRY naomba unisaidie. Nilipigwa na butwaa baada ya kugundua kua alikua ananitafuta mimi kwa muda wote, pia niliamini kua lile tabasamu lilikua la furaha ya kuniona baada ya kunitafuta kwa muda mrefu. Hii ni nafasi yangu pekee ya kuonyesha hisia zangu kwa mrembo huyo… je nitafanikiwa?... atanidharau kwa sababu mimi kapuku?.... au atanikubali ili nitimize ndoto zangu zilizokua zimekufa muda mrefu? Hayo na mengine mengi.. utayapata kwenye riwaya hii ya kusisimua. Enjoy..........