TE QUIERO MUCHO

TE QUIERO MUCHO

Imeandaliwa na:  Hussein Molito
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Mapenzi
Ukubwa : 26.14 kB

TEKIERO MUCHO Maneno matamu kutoka kwa malaika Na Hussein O. Molito 0718 97 56 59 / 0765 68 48 70 Introductions: Mapenzi ni safari ndefu ambayo mtu huianza bila kujua ni wapi ambapo anaweza kuishia. Kila mtu ana matamanio yake na vile alivyojiwekea mpenzi wake awe. Ndio maana inaweza kufikia hatua mtu ukatokea kumpenda kwa dhati mtu ambaye ana sifa mbaya sana mtaani kwao na ikafikia hatua hata mtu huyo akabadili tabia na kua mwema kabisa kama na yeye atakua na mapenzi ya kweli na wewe. Hata mimi sikudhania kama kuna siku moja nitasafiri hata kwenda nchi jirani tu kutokana na hali duni niliyokua nayo. Lakini katika hali ya sintofahamu. Nikakutana na mtoto mkali anayetokea nchini Hispania na kunifanya moyo wangu utamani kuwa nae. Hajui lugha ninayo izungumza. Hana urafiki na mtu yeyote wa karibu na mimi. Sina fedha nyingi za kuweza kumshawishi ili akubali kuwa na mimi kutokana na uwezo wa wazazi wake. Katika hali ambayo kila mmoja alikua hahitaji fedha, uzuri wa mtu au taifa alilotokea, ndipo mtoto mzuri akanitamkia nene la ushindi ambalo lilinipa nguvu na kunifanya nifumbue macho wakati yakikaribia kufumba kwa maumivu ya risasi kadhaa zilizoingia mwilini mwangu. Alikua analia sana na kuhisi yeye ndio chanzo cha kila kitu. Japo sikua nakijua vizuri kispanyola, lakini neno hilo nilijua maana yake kutokana na kulitamka kwa dhati ya moyo wake bila kufosiwa na mtu huku akinidhihirisha kua mimi ndio mwanaume wa maisha yake. “Tekiero mucho Molin. Aliongea maneno hayo na kunifanya nifarijike moyoni mwangu. “nakupenda pia Babra. Nilijibu huku nikimuonyesha tabasamu murua mtoto huyo ambaye alikua na hofu kubwa na maisha yangu kutokana na damu zilizokua zinanitiririka. HII AI YA KUKOSA.. NI STORY KAALI YA MAPENZI NA UTAIFURAHIA PIA.