DAR TO MUMBAI

DAR TO MUMBAI

Imeandaliwa na:  Nea Makala
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Mapenzi
Ukubwa : 123.07 kB

Siku zote kesho uandaliwa na leo, kama ukiitumia vyema leo yako basi hautokuwa na shaka kwa kesho uliyoiandaa leo, Mapenzi ni kama upepo na mwanadamu ni tiara, mapenzi yanaweza mpeperusha mwanadamu popote yapendavyo, kama ilivyo kwa tiara kupeperushwa na upepo, mapenzi yana uwezo wa kubadili na kuzima kabisa ndoto zako, nakumbuka bibi alishawahi nambia kuwa, “Usitegemee raha au furaha pindi tu uingiapo kwenye ulimwengu wa mapenzi, na kama ukihisi umependa basi uandae moyo wako kuumizwa, katika kiwango kile kile ulichopenda ndivyo ilivyo kwa moyo wako kuumia pale bahati itakapotoka upande wako”. Maneno hayo yakawa yanajirudia sana akilini mwa kijana mmoja ambae ni mfungwa katika jera moja iliyopo pembezoni kabisa mwa jiji la Delhi, afya ya mfungwa huyo ilidhoofika sana, kwani ni kwa muda mrefu alikuwa amefungiwa katika chumba kisichokuwa na mwanga hata kidogo kutokana na makosa aliyoyafanya, hakuelewa usiku upi na mchana ni upi, wala hakuweza tambua ni kwa muda gani amekuwa katika chumba kile. Kwa mara ya kwanza mlango wa chumba alichofungiwa kijana huyo mwenye asili ya kiafrika, ukafunguliwa na akatolewa nje ya chumba kile, kwa kumtazama unaweza kufikiri kuwa ni kikongwe cha miaka 70 ila ni kijana mdogo ambae ata miaka 30 hajafika. "Kutokana na mahusiano mazuri tuliyo nayo kati ya taifa letu na ardhi ya nyumbani kwenu, tunakupunguzia adhabu kuanzia sasa utatumikia kifungo chako ukiwa katika sero ya kawaida" Bwana jela aliwambia yule mfungwa wa kiafrika mwenye namba 117, "Ranjit embu mpeleke huyu hospitali, hakikisha anafanyiwa vipimo vyote na kurudishwa hapa", “Sawa mkuu,” alisema Ranjit ambaye ni mmoja kati ya askari jera. Baada ya mfungwa yule kufikishwa hospitali, daktari akaanza kumfanyia vipimo, huku akimuulza maswali kadhaa, lakini muda wote alikaa kimya asijibu lolote, "Mbona wewe si kiziwi wala bubu, kwanini hujibu ninavyokuuliza?" alisema Daktari huku akimkazia macho mfungwa, lakini asipate ushirikiano wowote. "Abdulrazak Kareem, mfungwa namba 117 Kwa makosa ya kigaidi na biashara haramu, naongea na wewe!" Daktari ambaye pia ni askari akajikuta akiongea kwa ukali kwa kutaja jina na makosa ya mfungwa anayemfanyia vipimo, baada ya miaka mingi kupita leo akili ya mfungwa ikafunguka na hakuamini kile alichokisikia toka kwa daktari, akalishangaa zaidi jina lile aliloitwa kwani alilifahamu kupitia vyombo vya habari akawa anajiulza zaidi imekuaje yeye kuitwa vile. "Abdulrazak Kareem! Kesi ya kigaidi na biashara haramu!? alijiuliza Mfungwa huku akishangazwa Sana japo alikuwa akitumikia kifungo kile hakuwa akijua ni makosa yapi hasa yaliyomueka hatiani.