TEARS OF AN ANGEL PART 1

TEARS OF AN ANGEL PART 1

Imeandaliwa na:  Hussein Molito
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Mapenzi
Ukubwa : 198.32 kB

TEARS OF AN ANGEL can you hear heaven cry? HUSSEIN O. MOLITO 0718 975659 / 0765 68 48 70 Nina kila sababu ya kuyatoa machozi yangu kukulilia wewe. Naumia kila siku kila nikufikiriapo. Ni sawa na uzito wa jabali kubwa lilio angukia kwenye kifua cha binaadamu mwenye ndoto za kuyaokoa maisha yako. Nilitamani kukusogelea Zaidi ya hapa. Umewahi sana. Ungenipa hata dakika moja tu ya kuongea na wewe. Labda kauli yangu ingeweza kubadilisha mueleko wako. Umepotea kama mawingu mekundu yapoteavyo pindi kiza kiingiapo. Sikuwahi kukuambia wewe ndio bora kwa sababu ubora wako unajieleza. Lakini kwakua hukuisikia sauti yangu uikisema, ukaamua kujiondoa thamani. Kla mtu anakulilia. Kla mtu anaumia…kkla mtu anajutia…dah, ni kweli Ulikua kipenzi cha wengi. Kipenzi cha kila mpenda filamu. Ulikua Super Star…..nyota mkubwa hapa nchini kwetu. Uliipeperusha bendera na kila mtu alitamni kuwa kama wewe siku moja. Lakini ubongo wako ukashindwa kupepumbua kipi kilichotoa mwanga kati ya tochi na betri. Hakika fumbo la maisha yako limefumbuka haraka kuliko lilivyofumbwa. Najua unanisubiri, japo sijui ni lini nitakuja. Pengine labda ulikua na swali ulitaka kuniuliza lakini ulishindwa kutokana na muda kuzidiwa mbio na tamaa iliyokupata kwenye kichwa chako. Kwangu mimi naweza sema kua halikua tamanio sahihi. Laiti kama ningejua klichopo kwenye mfumo wa ubonngo wako, angalau ningeweza kutumia njia yoyote kukuzuia. Lakini kwa sasa kila kitu kimebaki historia. Uliniahidi utakuja tena kwenye filamu nyingine. Filamu inayohusu maisha yetu. Mbona umeikatisha? Hivi hukufikria kua wewe ndio mboni yangu.? Kwanini umeamua kufanya hivyo? Kwanini umeamua kunifanya kuwa mtu wa kulia kra mara?...hivi unakisikia kilio changu?..mbona hunijibu?..nijibu basi ili moyo wangu utulie, pengine unijibie swali langu linalonifanya nijione mwenye hatia kila nikikufikria. hivi ni kweli mimi ndio sababu ya yote haya kutokea? Kama ni hivyo kwanini hukuniambia? … ningeacha kla kitu kwa sababu yako…. Inaniuma sana…… kama huko ulipo kuna maisha mengine Zaidi ya haya…nakutakia maisha mema huko ulipo. PATA LADHA KAMILI KWENYE RIWAYA HII ITAKAYOKUTOA MACHOZI