RUDI (VOLUME 2)

RUDI (VOLUME 2)

Imeandaliwa na:  Hussein Molito
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Maisha
Ukubwa : 166.10 kB

RIWAYA : RUDI NA HUSSEIN O. MOLITO MAWASILIANO O718 97 56 59 0765 68 48 70 UTANGULIZI: Kila nikitazama mawingu, nahisi yananizomea na kunilaumu. Hata Ardhi pia inanisuta na kunilaumu. Najiona mkosaji kuliko viumbe vyote hapa duniani. Kila kitu nahisi kinanichukia. Nahisi dunia hainipendi tena na inatamani ningetoweka kwenye uso wake. Machozi pekee hayawezi kunipunguza machungu niliyoayo moyoni mwangu. Machozi hayawezi kunisahaulisha kumbukumbu za makosa niliyowafanyia watu wasio na hatia hata kidogo. Hakika majuto ni mjukuu. Wakati natenda sikuwahi kufikiria kua mwisho wake utafika. Mwisho wenye fadhaa kubwa na kunifanya niyakimbie makazi ambayo nilikua Napata kila ninachokihitaji. Makazi ambayo nimetokea kupendwa kuliko watoto halisi wa familia husika. Sijajua ni kipi kilichoiponza nafsi kati ya Balehe au nyeti zangu. Sijui ni lana ya msichana niliyempa ujauzito na kuikana kuilea? Hakika kila nikiyahesabu makosa yangu yote niliyo yafanya kwa watu nagundua kua mimi sio binaadamu na nastahili hata kuzikwa hai kwa dhambi nilizotenda. Nimerudi katika maisha mabovu zaidi ya yale niliyokua naishi mwanzo. Sina baba, sina mama. Ninapoishi hakuna maadili wala sheria. Nimeshashuhudia mwanaume mwenzangu akifanywa vibaya na wanaume wenzake. Nimeshashuhudia watu wakichomana visu kisa wamedhulumiana shilingi mia tano. Kila mtu nimuonaye amevurugwa na maisha na anaweza kufanya kitu chochote bila aibu. Hakika ni maisha mabovu niliyojitakia mwenyewe kuishi na kuacha maisha ya kifahari ya watu waliojitolea kwa moyo wote kunihamisha kwenye maisha haya ya ajabu. Natamani kurudi lakini uso umeumbwa na haya. Hakika siwezi kurudi tena kwa kile nilichokitenda juu yao. Wakati mwengine natamani kuwaomba msamaha, ila nahofia kuuwawa hata kabla sijalitamka neno hilo. Kama nitapewa nafasi ya kuchagua kitu gani kirudi, basi ningechagua miaka irudi nyuma ili nisafishe kila kosa nililolifanya. HAYA NA MENGINE MENGI UTAYAKUTA KWENYE RIWAYA YA RUDI