KICHWA CHAKO

KICHWA CHAKO

Imeandaliwa na:  Kalmas Konzo
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Upelelezi
Ukubwa : 323.16 kB

Hujuma kubwa sana inafanywa katika nchi ya Bantu, Virusi wenye kusababisha ugonjwa wa ajabu wanapandikizwa katika mji wa Kintu na kusababisha vifo vya wananchi wengi Mkemia mkuu wa serikali Dr. Charles anafanya utafiti na kugundua tatizo la ugonjwa ule pamoja na formula ya tiba ya ugonjwa ule. Formula ile inasakwa kwa udi na uvumba na watu wenye nia mbaya wakiwemo viongozi wakubwa wa serikali. Jambo hili linapelekea Dokta Charles kuuawa. Formula ile anakabidhiwa Sammy mdogo wa Dokta Charles kabla ya kifo cha Dokta Charles. Sammy anaanza kusakwa kwa udi na uvumba ili formula ile iweze kuporwa. Je, sammy atakamatwa? Sasa ungana nami kwa kupakua goma hili la kibabe uone jinsi simulizi hii ilivyoandikwa kwa kutumia akili kubwa. Hakika ukianza kuisoma tu, hutaacha mpaka mwisho. Twende sawa sasa!