KWA SABABU NAKUPENDA

KWA SABABU NAKUPENDA

Imeandaliwa na:  Frank Masai
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Mapenzi
Ukubwa : 232.55 kB

Kutana na Daniel Lungwa na Josephine Malinzi. Vijana waliyosoma pamoja shule ya sekondari. Josephine akiwa mtoto wa mkuu wa shule ambayo wanasoma na Daniel, anajikuta akizama kwenye mapenzi na Dannie. Naye Daniel anakufa na kuoza, lakini kikwazo kinakuja kuwa baba yake Josephine. Hataki kabisa kusikia mwanaye anaanzisha mahusiano. Hapo ndipo Daniel anawashiwa moto hadi anashindwa kufanya mitihani yake ya kidato cha nne. Malengo ya Daniel ya kusoma hadi chuo yanakufa. Anaamua kuwa mwendesha bajaji na wakati huo Josephine anafika hadi chuo na anapata mpenzi mpya. Lakini mpenzi huyo mpya, aanakuwa si kitu kwa Josephine hasa pale anapokutana tena na Daniel (Baada ya miaka sita ya kupotezana). Mapenzi yao yanarudi tena, lakini kama kawaida, baba wa Jose anaingilia kati. Soma mkasa huu wa kukata na shoka.