DEMU WA FACEBOOK

DEMU WA FACEBOOK

Imeandaliwa na:  George Mosenya
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Mapenzi
Ukubwa : 206.93 kB

Kituo cha mabasi yaendayo Tegeta kilikuwa kimesheheni watu kama ilivyo kawaida. Magari yanayoishia Magomeni hayakuwa katika kashkashi yoyote ile na wala yale yaendayo Kariakoo pia hayakuwa katika suluba ya kugombewa kama yalivyokuwa yale ya Tegeta. Katika kituo hicho cha Kinondoni Biafra umati wote uligeuka kuwa na hulka ya aina moja. Gari likija wote wanageuka kuwa wanariadha. Na wanapoufikia mlango wa gari wanageuka kuwa mabondia kwa jinsi wanavyougombea mlango mmoja wa gari aina ya DCM. PAKUA SIMULIZI HII KUENDELEA....