THE GIRL IN ISLAND 2

THE GIRL IN ISLAND 2

Imeandaliwa na:  Hussein Molito
Gharama (TSHS.) : FREE
Kundi : Uchawi
Ukubwa : 68.61 kB

THE GIRL IN ISLAND SEASON II (INTODUCTION) WITH HUSSEIN O. MOLITO 0718 97 56 59 Baada ya siku chache kupita nikitokea kwenye kisiwa cha wanawake kilichojaa maajabu na mauza uza yatishayo, hatimaye ilifikia muda wa kurudi huko kwa ajili ya kuhalalishwa msichana niliyerudi naye kutokea huko kama mke wangu rasmi. Mwanzoni nilitaka kugoma kurudi kwa jinsi tulivyopata tabu ya kukitoroka kisiwa hicho, ila ujasiri wa mke wangu mtarajiwa uliniondoa hofu na kujikuta nakua tayari kurudi kisiwani humo ambapo kwa miaka takribani hamsini na zaidi, hakuna mtu ambaye alienda huko akafanikiwa kurudi zaidi yangu. Nilijipa imani kua kama nitakua beneti na msichana huyo aliyetokea kunipenda na kuniokoa mara kadhaa katika midomo ya vifo iliyokua inanitamani kila dakika. Baada ya kuingia kwenye maji tayari kwa kurudi huko kisiwani, nilipatwa na mshtuko baada ya msichana huyo kuniambia kua tunatakiwa kujiachia kwenye maji kuna sehemu alikua ana hitaji tuende kabla ya kurudi kisiwani. Wakati najadili kichwani kwangu juu ya uamuzi huo wa ghafla wa mpenzi wangu, nilijikuta nipo ndani ya maji taratibu nazama huku yeye akiwa amenishika mkono. Nilijitahidi kubana pumzi na hatimaye nilijikuta naachama kutokana na kushindwa kujizuia. Nilipigwa na butwaa baada ya kuona yale maji hayaingii mdomoni mwangu. Na hata nilipojaribu kuvuta pumzi, niliweza kuvuta vizuri tu bila kupata shida yoyote. Nilishindwa kuelewa ni vipi binaadamu wa kawaida anaweza kupumua na kufanya chochote chini ya maji bila kutumia kifaa chochote?, ila jibu lilikua ni mtu niliyekua naye hakua ni binaadamu wa kawaida. Bali alkua ni jinni. Hiyo safari anayonipeleka, ni wapi? Na kwa nani? Na mbona hakuniambia toka mwanzo kama kuna safari ya chini ya maji? Nini dhamira yake ya kung`ang`ania kurudi kwenye kisiwa cha MALAIKA wakati tuliondoka tukiwa tumeacha mauaji ya malikia wao? Na kama tukifika huko, watatupokea vipi? Je wazazi wake hawatakua wameshambuiwa na wananchi huko kwa kitendo chake cha kumuua malikia wa mwanzo? FUATILIA SASA..........